![]() |
Mwanafunzi asiyeona, Winfrida Gilbert Wilson, Juni 7, 2026 amekwenda kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mujibu wa Sheria katika Kikosi cha Ruvu JKT kilichopo Mlandizi, mkoani Pwani.
Hatua hiyo ikiwa ni mwendelezo wa safari yake ya elimu na maendeleo baada ya kuhitimu Kidato cha Sita kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto ya kutokuona.
Winfrida amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuendelea kumpatia msaada na kumtia moyo katika safari yake ya elimu. Amesema msaada huo umekuwa nguzo muhimu katika mafanikio yake na umempa ari ya kuendelea kupambana ili kufikia malengo yake ya kielimu na maisha kwa ujumla.
Aidha, Winfrida ameahidi kutumia vyema kipindi cha mafunzo ya JKT kwa kujifunza mambo mbalimbali yatakayomjengea uwezo, nidhamu, uzalendo na stadi za maisha. Amesema yuko tayari kujifunza na kupata uzoefu mpya utakaomsaidia katika maisha yake ya baadaye, huku akiahidi kuwa balozi mzuri wa vijana wenye mahitaji maalum kwa kuonyesha kuwa ulemavu si kikwazo cha kufikia mafanikio.


Post a Comment