WANANCHI MBANGALA WAHIMIZWA KUTATUA MIGOGORO KWA NJIA YA AMANI

.Wakazi wa Kata ya Mbangala, Wilaya ya Songwe mkoa Songwe, wametakiwa kutatua migogoro inayojitokeza katika familia na jamii zao kwa kushirikisha viongozi wa vijiji na kata ili kupunguza vitendo vya uhalifu vinavyotokana na kulipiza visasi baina ya wanajamii.


Akizungumza na wananchi hao tarehe 08 Juni 2026, Polisi Kata wa Mbangala, Mkaguzi wa Polisi Peter Sulemani, aliwahimiza wazazi na walezi kuzingatia malezi bora kwa watoto kwa kuhakikisha wanapata elimu na lishe bora ili kuwajengea afya njema na kuwaandaa kuwa raia wema wa baadaye.


Aidha, Mksguzi Selemani aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudumisha amani na usalama kwa kutoa taarifa za wahalifu na vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza maana ushirikiano wa wananchi na Jeshi la Polisi ni muhimu katika kuwabaini na kuwachukulia hatua wahalifu kwa manufaa ya jamii nzima.


Post a Comment

Previous Post Next Post