Mshambuliaji tegemeo na nyota wa klabu ya Fulham inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Rodrigo Muniz amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya mapumziko yake ya kiangazi baada ya kumalizika kwa msimu wa soka kule barani Ulaya.
Mshambuliaji huyo raia wa Brazil ametumia ukurasa wake wa Instagram kushare picha inayomwonyesha akiwa ndani ya gari maalum la utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Muniz amesindikiza picha hizo kwa ujumbe mfupi unaosomeka “African Vibes!” huku akiweka emoji ya bendera ya Tanzania .


Post a Comment