Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, Machi 2, 2026 amefanya ziara Mkoani Pwani katika kiwanda cha Keds Tanzania Co. Ltd kinachozalisha bidhaa za usafi pamoja na kiwanda cha Aluminiam Trailers Limited kinachozalisha Matera (Trailers) ya Malori.
Aidha, Lengo la ziara hiyo ilikuwa kufuatilia utekelezaji wa Sheria mbalimbali za Kazi ikiwemo Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Mwaka 2003.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge alipofanya ziara iliyolenga kukagua utekelezaji wa Sheria za Kazi ikiwemo Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya Mwaka 2003 katikamaeneo mbalimbali ya kazi katika mkoa huo tarehe 2 Machi, 2026.




Post a Comment