Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Happiness Ngwando tarehe 03 Machi, 2026 ametembelea Shule ya Msingi Semeni iliyopo Wilaya ya Tunduru ikiwa ni baada ya kuwachimbia Kisima cha Maji ambacho kimegharimu Shilingi 7,800,000 kitakachowasaidia Wanafunzi na Walimu kutotembea umbali mrefu kutafuta maji.
Mbunge Happiness Ngwando anaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuendelea kuwachimbia visima Wananchi.
Akizungumza na Wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi Semeni, Mhe. Happiness Ngwando amewaomba kutunza miundombinu ya maji ili iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
*#KazinaUtuTunasongaMbele*


Post a Comment