Mh.Masache N.Kasaka- Mbunge Jimbo la Lupa ameshiriki kukagua ujenzi wa daraja la Lupatingatinga ambapo lilishakamilika na limeanza kutumika na mkandarasi aliyekuwa akitekeleza ni Summer Communication LTD kwa gharama ya shilingi 5,671,801,051.88
Sambamba na hilo Mh. Kasaka amemshukuru Rais *Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan* kufanikisha ujenzi huo ikiwa ni ishara ya ujio wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami kutoka Makongolosi kuelekea Rungwa hadi Mkiwa.
Katika ziara hiyo iliongozwa na Kaimu RC Mbeya *Brigedia Jenerali Maulid Surumbu* Mkuu wa wilaya Mbarali na viongozi wengineo walioshiriki ni Mkuu wa Wilaya Chunya *Mh.Batenga*,Wakurugenzi wa halmashauri,Wah Wabunge *Mh.Shida Patali* Mbunge wa Mbeya Vijijini, *Mh.Merryprica W.Mahundi* Mbunge viti Maalumu Mkoa Mbeya na Naibu waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu na wataalamu kutoka ofisi ya Tanroad mkoa na wilaya.
*KAZI NA UTU CHUNYA TUNASONGA MBELE*




Post a Comment