Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii 18 Machi 2026 imetembelea na kukagua mradi wa mfumo wa kielektroniki wa utatuzi na usuluhishi wa migogoro (e- UTATUZI) unaotekelezwa na Tume ya Usuluhuhishi na Utatuzi wa Migogoro (CMA) ziara iliyofanyika Dar es Salaam ambapo imepongeza Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Ajira na Mahusiano kwa jitihada za kuwaondolea kero wananchi kupitia mfumo huo ulioanza kuonesha mafanikio tangu ulipozinduliwa Januari mwaka huu.
Aidha, Kamati hiyo imekamilisha ziara yake leo kutembelea miradi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano iliyoanza 11 Machi 2026 ambapo ilikagua miradi kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Dar es Salaam.


Post a Comment