Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeipongeza serikali kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa bwawa la Kidunda unaotekelezwa na wizara ya maji chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) mradi unaotarajiwa kutatua kero ya uhaba wa maji katika Jiji la Dar es salaam, Pwani na maeneo mengine yanayohudumiwa na DAWASA hasa katika kipindi cha kiangazi.
Bwawa la Kidunda linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kuweza kuhifadhi lita bilioni 190 za maji ambazo zinakidhi mahitaji ya maji kwa kipindi cha kiangazi.
Mradi huu unagharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 335.87 kwa ufadhili wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.
Wajumbe wa kamati wameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi na kuisisitiza wizara ya maji kuhakikisha mkandarasi anakamilisha kazi za ujenzi kwa wakati kama ilivyo katika mkataba ambapo mradi huu unatarijiwa kukamilika Disemba 2026.
Katika ziara hiyo Wajumbe wakamati wakiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Jackson Kiswaga walipokelewa na kuongozwa kuelekea eneo la mradi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Bi. Rose Ambrosi pamoja na watendaji wa wizara ya Maji.




Post a Comment