*MHE. KWAGILWA AHIMIZA WAZAZI KUTOA KIPAUMBELE CHA ELIMU KWA WATOTO

*aibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Reuben Kwagilwa amewaomba wazazi, walezi na viongozi wa dini nchini kuwahimiza watoto kwenda shule akisisitiza kuwa urithi pekee anaoweza kupewa mtoto ni elimu.


Mhe. Kwagilwa ameyasema hayo Machi 19,2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la Handeni Mjini wakati wa Iftar aliyoiandaa nyumbani kwake eneo la Kwenjugo wilaya ya Handeni mkoani Tanga, katika kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani.


“Kwa sasa Watanzania tunakaribia milioni 70, hii ina maana kubwa kuwa Watanzania tumeongezeka sana lakini ardhi haijaongezeka. Kila mahali ambako tumeenda na kufanya mikutano, mkiitisha kero za wananchi asilimia 80 ya kero hizo ni ardhi, ndio maana nasema urithi pekee tunaoweza kuwapatia watoto wetu ni elimu,” amesema Mhe. Kwagilwa.


Amesisitiza kuwa mabadiliko ya sera yameifanya elimu ya kidato cha nne kuwa sehemu ya elimu ya msingi, hivyo kisheria watoto wanapaswa kusoma hadi kufikia angalau kidato cha nne na kuendelea.

Aidha, Mhe. Kwagilwa ametumia jukwaa hilo 

kwashukuru wananchi wa Handeni kwa imani kubwa walioionesha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2025, imani ambayo imemuamini mbunge wao na kumteua kuwa msaidizi wake kwa nafasi ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI anayeshughulikia Elimu.

Post a Comment

Previous Post Next Post