OWM - TAMISEMI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Florent Kyombo, Machi 20, 2026 imepitisha mipango na bajeti za mikoa minne kwa mwaka wa fedha 2026/27 baada ya kupitia na kujadili kwa kina mapendekezo yaliyowasilishwa.
Katika kikao hicho, mikoa ya Shinyanga, Manyara, Singida na Dodoma iliwasilisha rasmi mipango yao mbele ya kamati, ambapo wajumbe walisisitiza umuhimu wa utekelezaji wenye tija ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Aidha, imeelezwa kuwa maandalizi ya mipango na bajeti hizo yamezingatia nyaraka muhimu za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2026/27–2030/31), Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030.
Kamati imepongeza hatua hiyo na kusisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti katika utekelezaji wa mipango hiyo ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati na kuleta maendeleo endelevu nchini.





Post a Comment