Afariki baada ya kuingia na cheni ya chuma kwenye kipimo cha MRI.

Mwanaume mmoja huko New York Marekani amepoteza maisha baada ya kuvutwa na sumaku alipoingia kwenye kipimo cha MRI. Adrienne Jones-McAllister ambaye ni mke wa marehemu amevieleza vyombo vya habari kwamba siku ya Jumatano wiki iliyopita yeye (mwanamke) alikuwa anafanyiwa kipimo cha MRI ya goti, baada ya kipimo kumalizika alimwita mume wake aingie kwenye kipimo ili amsaidie kuinuka kutoka kwenye kitanda. 

Mwanaume huyo aliingia kwenye chumba cha MRI akiwa na mkufu wa chuma shingoni uliokuwa na kufuri lenye uzito wa kilo 9 ambalo huwa analitumia kupiga mazoezi, ndipo mwanaume huyo alipovutwa na sumaku na kupoteza maisha baadae. Mwanaume  huyo alikuwa na umri wa miaka 61.

 Kipimo cha MRI kinatumia sumaku ili kutoa picha za sehemu mbalimbali za mwili. Baadhi ya mashine za MRI zina sumaku yenye uwezo hata wa kuvuta gari yenye tani 10.

 Nguvu ya sumaku huwa ipo muda wote hata kama hakuna mgonjwa kwenye kipimo. Kwa kawaida mgonjwa au ndugu wa mgonjwa au wahudumu wenyewe hawapaswi kabisa kabisa kuingia au kuingiza kitu chochote chenye chuma wanapoingia kwenye kipimo cha MRI. 

Mwaka 2001 huko huko Marekani mtoto alipoteza maisha baada ya mhudumu kuingia na mtungi wa Oxygen uliovutwa na kupasua kichwa cha mtoto. 

Mwaka 2023 huko Brazil mwanaume mmoja alifariki dunia baada ya kuingia na bastola kwenye kipimo cha MRI, bastola hiyo ilivutwa na kisha kufyatuka na risasi kumpiga mwanaume huyo!

Post a Comment

Previous Post Next Post