Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited ulioongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake Bi. Julia Evelyn Morley.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited ulioongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake Bi. Julia Evelyn Morley, Mshindi wa Miss World 2025 Bi.Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand,  Miss World Africa Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia, Kizimkazi Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025. 


Pia kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, pamoja viongozi wa Maliasili na utalii. Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili namna ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Miss World 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 Bi. Opal Suchata Chuangsri mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025.
@ikulu_mawasiliano

Post a Comment

Previous Post Next Post