MKURUGENZI MKUU WA TCRA AKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO KIGOMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari amekutana na kuzungumza na Watoa Huduma za Mawasiliano wenye leseni za huduma za Utangazaji ikiwemo maudhui ya redio, televisheni na mtandaoni, pamoja na huduma za intaneti kutoka mkoa wa Kigoma, tarehe 19 Mei 2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya Mkurugenzi Mkuu na wateja wa TCRA anayofanya kila kanda na ofisi ya Zanzibar. Mkutano huo umejadili masuala mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya Mawasiliano, ikiwemo kupokea maoni, ushauri na changamoto kutoka kwa watoa huduma hao; ambapo ufafanuzi wa hoja zote umetolewa na Mkurugenzi Mkuu, pamoja na Meneja wa Ofisi ya TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salumu.


Katika kuchagiza usimamizi thabiti wa sekta ya Mawasiliano, TCRA hutumia dhana ya usimamizi kwa mashauriano na hukutana mara kwa mara na wadau wa sekta wakiwemo watoa huduma, ili kuhakikisha mustakabali bora wa ukuaji wa sekta pamoja na matumizi chanya ya fursa zinazoletwa na ukuaji wa teknolojia kwa maendeleo ya utoaji wa huduma za utangazaji, posta pamoja na simu na intaneti.

@tcra_tanzania 


#tcratz #elimukwaumma #mikutanonawadauwasektayamawasiliano #sektayautangazaji #sektayaposta #sektayasimunaintaneti

Post a Comment

Previous Post Next Post