Mhe. Bashiru ameyasema hayo leo, katika ziara yake ya kikazi katika Kijiji cha Lemooti, Kata ya Lemooti, Wilaya ya Longido, Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa wazee wa kimila wanaushawishi mkubwa katika jamii hiyo, hivyo ni vyema wakawashirikisha na Jeshi la Polisi katika ya kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia wizi wa mifugo katika maeneo yao.
Akizungumzia migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, Waziri Bashiru amesema kuwa migogoro hiyo imekuwa ikisababishwa na uratibu mbaya wa matumizi ya ardhi pamoja baadhi ya wasimamizi wa sheria kutokuwa waadilifu, hivyo ni vyema viongozi wa serikali pamoja na wanajamii wakashirikiana kwa pamoja katika kutafsiri sheria za matumizi sahihi ya ardhi.
Aidha Waziri huyo pia amewasisitiza wafugaji hao kuzingatia ufugaji wa kisasa ambao utachangia kuongeza tija kwao na hatimaye kupunguza kero ambazo hutokana na ufugaji wa kiasili katika maeneo mbalimbali Nchini.






Post a Comment