Matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia na watoto wilaya ya Gairo mkaoni Morogogo yatajwa kuwa sababu ya wananchi na wadau wa maendeleo kuanzisha ujenzi wa jengo maalumu litakaloshughulikia makosa hayo.
Akitoa taarifa mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Mkuu wa Polisi jamii wilaya ya Gairo ASP Minael Senzige amesema ujenzi huo ulianza machi 3, 2024 kwa nguvu kazi ya wananchi, ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Mbunge wa jimbo la Gairo ambapo mpaka hatua hiyo umegharimu kiasi cha shilingi 23,696,000/=
Mara baada ya kulikagua jengo hilo, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu Wazo Michael Mwan'gonda amesema, ameridhishwa na ubora wa jengo hilo na kutoa pongezi kwa wananchi pamoja na wadau wa maendelo huku akiwataka waendelee kuwa karibu na Jeshi la Polisi ili kushirikiana katika kulinda amani na utulivu.


Post a Comment