Leo 21 Aprili 2026, Mbunge Ezra John Chiwelesa ameibana serikali bungeni kuharakisha upelekaji wa huduma ya mawasiliano katika Kata ya Nyabusozi na Kijiji cha Migango kata ya Runazi.
Ameeleza kuwa ukosefu wa mtandao unaathiri shughuli za kiuchumi, upatikanaji wa taarifa na huduma za kijamii, akisisitiza mawasiliano ni hitaji la msingi kwa zama hizi.
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama (Mb) imekiri changamoto hiyo na kuahidi utekelezaji wa haraka kupitia mpango wa dharura ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo bila kuchelewa.


Post a Comment