WAZIRI MKUU, DKT. NCHEMBA AWATAKA WASHITIRI KUFANYA UTAFITI KABLA YA KUSAMBAZA TAARIFA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kuhakikisha wanafanya utafiti wa kutosha kabla ya kusambaza taarifa kwa umma.


Amesisitiza kuwa utafiti ni msingi wa kutoa taarifa sahihi, zinazoeleweka na zenye kuaminika kwa jamii.


Ameongeza kuwa ni muhimu watayarishaji kuwasilisha maudhui wanayoyaelewa vizuri ili kuepuka upotoshaji na kuongeza ufanisi wa mawasiliano.


Waziri Mkuu ametoa wito huo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 110 wa Watayarishaji wa Vipindi vya Elimu kwa Umma (WASHITIRI) 2026, ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu kwa umma.


Mkutano huo unafanyika katika Jengo la PAPU jijini Arusha.


Mdhamini Mkuu wa mkutano huo ni PSSSF pamoja na NSSF.


WAKATI HUO HUO; WAZIRI MKUU ATOA WITO KWA WASHITIRI KUSHIRIKISHA VIJANA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kuandaa maudhui yatakayowafikia na kuwagusa vijana kwa lugha wanayoielewa.


Amesema bila kutumia njia na lugha rafiki kwa vijana, taarifa muhimu zinaweza zisifikie walengwa au kushindwa kuwavutia.


Waziri Mkuu amesisitiza kuwa maudhui yanapaswa kuwa sahihi, ya kuvutia na yenye thamani ili vijana waweze kuyapokea na kufurahia kuyafuata.


Waziri Mkuu ametoa wito huo jijini Arusha leo Machi 25, 2026, wakati wa ufunguzi mkutano wa 110 wa Watayarishaji wa Vipindi vya Elimu kwa Umma (WASHITIRI) 2026 ambo umeandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu kwa umma.


Mdhamini Mkuu wa mkutano huo ni PSSSF pamoja na NSSF.

Post a Comment

Previous Post Next Post