Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Ado Shaibu Ado imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi miwili ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza ambapo imekagua ujenzi wa jengo la Osisi za Utawala la na Shule ya Sekondari ya Magu Mjini.
Katika ziara hiyo, Kamati iliambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Mkoa wa Mwanza, wakiongozwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Mhe. Reuben Kwagilwa akiwa sambamba na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene.
Kamati hiyo imesisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na thamani halisi ya fedha ili iweze kuwanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.


Post a Comment