Rais Samia kupitia ujumbe wake wa Siku ya Wanawake March 08,2026, amesema “Kauli mbiu hizo zinatukumbusha kwamba maendeleo ya kwell ya jami na Taifa letu yanajengwa katika msingı wa haki na sawa na ushirikishwaji, pamoia na moyo wa kujitoa, kushirikiana na kuwainua wengine, kwa asili, Mwanamke ni Mama, ni Mlezi, ni Kiongozi na ni Mfariji wa familia, jamii na Taifa.
“Katika maisha ya kila siku, Wanawake wanaishi kwa vitendo falsafa ya "Kutoa ndiyo Kupata", wanajitoa kwa Familia zao, wanalea kizazi, wanahudumia jamii na wanachangia kwa namna mbalimbali maendeleo ya Taifa letu, hata katika nyakati za changamoto, Mwanamke hakimbii majukumu, badala yake, hubeba changamoto hizo kwa ujasiri na hekima, na kuzigeuza kuwa nguvu ya kuimarisha familia, jamii na Taifa.


Post a Comment