Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amepokea Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi iliyotengewa Fedha katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Taarifa hiyo imewasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. William Lukuvi leo tarehe 09 Machi 2026, katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Baadhi ya Miradi iliyowasilishwa ni pamoja na Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), Ujenzi wa Kiwanda cha uchapishaji wa Nyaraka za Serikali, Mradi wa Kuimarisha uwezo wa Nchi katika Kujiandaa na kukabiliana na Maafa, Mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar na Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Taifa cha Utengamao.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu Dk. Jim Yonazi, Naibu katibu Mkuu Dkt. James Kilabuko wa Ofisi hiyo na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri (SBUU).









Post a Comment