KAMATI YA BUNGE YA PIC YARIDHISHWA NA MRADI WA NYUMBA WA TBA - CANADIAN MASAKI


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi wa Canadian Village uliopo Masaki, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Masanja Kadogosa, amesema kamati imejiridhisha kuwa thamani ya fedha iliyowekezwa inaendana na ubora wa majengo hayo. “Sisi kama kamati tumejiridhisha kwamba ukiangalia thamani ya fedha iliyowekezwa na majengo yenyewe, unaona thamani halisi ya fedha,” alisema Kadogosa.


Aidha ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo unaendana na maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Ilani yake, inayosisitiza kuboresha sekta ya makazi, hasa katika miji inayokua kwa kasi. Mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo matatu ya makazi, ambapo kila jengo linagharimu shilingi bilioni 4.6 na lina uwezo wa kuchukua familia 12

Post a Comment

Previous Post Next Post