Tarehe. 07/12/2024
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera *Comrade Faris Buruhani,* ameongoza uzinduzi na makabidhiano ya nyumba ya Mama Asimwe sambamba na chumba kimoja cha biashara. Tukio hilo limefanyika leo tarehe 07/12/2024 katika kata ya Izigo, wilaya ya Muleba.
Makabidhiano hayo yamekuja baada ya ukamilishaji wa ahadi ya Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Kagera kwa Mama Asimwe, ya kumboreshea mazingira yake ya kuishi kwa kumjengea nyumba ya kuishi na chumba kimoja cha biashara.
Ni miezi 6 sasa imepita tangu tukio la ajabu na la kikatili la Mauaji ya Mtoto asiye na hatia Asimwe Novat, aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (Albino) litokee na kuacha simanzi kubwa kwa mwana dada Judith Richard (Mama Asimwe) na jamii nzima ya watanzania.
![]() |
Chanzo @CCM Page
Post a Comment