Ifahamu Barabara ya Kimataifa ya Kasulu Mjini na Manyovu (kilometa 68.24) inayounganisha Tanzania na Burundi.

Barabara ya Kimataifa kati ya Kasulu Mjini na Manyovu (Kilometa 68.24) inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami kuunganisha Tanzania (Kigoma) na Burundi.
Hii ni miongoni mwa barabara za Kimkakati zinazoendelea kujengwa nchini Tanzania katika kukuza ushirikiano wa kimataifa na kurahisisha huduma za uchukuzi kati ya Tanzania na Burundi. Barabara hii pia inarahisisha shughuli mbalimbali za kila siku za kichuuzi kwa wakazi wa Kigoma.
Mradi huu, ambao umegawanyika katika hatua nne, kwanza ni Manyovu - Kasulu (Kilometa 68.25), pili ni Kidyama-Mvugwe (Kilometa 70.5), tatu ni Mvugwe – Nduta (Kilometa 59) na nne ni Nduta-Kabingo (Kilometa 62.25), unatarajia kukamilika mnano Machi 2025.
Chanzo @ Kigoma Region Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post