Vijana na wananchi wa Kitongoji cha Chang'ombe, Kata ya Kabuku Ndani, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kutojichukulia sheria mkononi na kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Akitoa elimu hiyo tarehe 13 Juni 2026 katika Kitongoji cha Chang'ombe, Polisi Kata wa Kabuku Ndani, Insp. Abdallah, aliwahimiza wananchi kuwa watulivu pindi matukio ya kihalifu yanapotokea na kuepuka tabia ya kuwashambulia watuhumiwa, badala yake wawakamate na kuwafikisha katika vituo vya polisi kwa mujibu wa sheria.
Aidha, wananchi hao walielimishwa umuhimu wa kutoa taarifa za uhalifu kwa wakati kwa Jeshi la Polisi ili kuwezesha hatua za haraka kuchukuliwa, kuhifadhi vielelezo vya ushahidi na kufanikisha uchunguzi pamoja na ukamataji wa wahalifu.





Post a Comment