Video- RAIS SAMIA AFUNGUA JUKWAA LA BIASHARA TANZANIA-URUSI JIJINI ST. PETERSBURG, ATOA WITO WA UTEKELEZAJI BADALA YA MAZUNGUMZO PEKEE

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 05.06.2026.

amefungua rasmi Jukwaa la Biashara Tanzania-Urusi jijini St. Petersburg na kutoa wito

kwa wawekezaji, viongozi wa biashara na taasisi kutoka nchi hizo mbili kutafsiri urafiki

wa muda mrefu kuwa ushirikiano halisi wa kiuchumi na uwekezaji.


Akilihutubia Jukwaa hilo lililofanyika pembezoni mwa Jukwaa la 29 la Kimataifa la UUchumila St. Petersburg (SPIEF 2026), Rais Samia alisisitiza kuwa Tanzania na Urusii zimekuwaa uhusiano imara wa kidiplomasia kwa zaidi ya miongo sita, lakini akabainisha kuwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara bado haujafikia uwezo wake kamili.

“Kiwango cha sasa cha biashara kati ya Tanzania na Urusi hakiendani na hadhi ya uhusiano wetu wa pande mbili. Hapa si mahali tunapopaswa kuwa,” alisema Rais Samia.


Rais Samia amesema kuwa licha ya nchi hizo mbili kujenga msingi imara wa kuaminiana na kushirikiana kwa miaka mingi, sasa umefika wakati wa kuelekeza nguvu katika matokeo ya vitendo, kuongeza uwekezaji na kupanua biashara.

Dkt Samia alieleza kuwa Jukwaa hilo ni fursa muhimu kwa jumuiya za biashara za Tanzania na Urusi kuzungumza moja kwa moja, kutambua fursa zilizopo na kujenga ushirikiano utakaotoa manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi wa nchi hizo mbili.


Akizungumza awali katika Jukwaa hilo, Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi, Mheshimiwa Maxim Reshetnikov, aliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa washirikawenye fursa kubwa zaidi kwa biashara za Urusi barani Afrika kutokana na ukuaji wake imara wa uchumi, utajiri wa rasilimali asilia, idadi kubwa ya vijana na nafasi

yake ya kimkakati kama lango la masoko ya kikanda.


Post a Comment

Previous Post Next Post