Wito huo umetolewa leo Juni 15, 2026, na Mkuu wa ushirikishwaji jamii kutoka Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Juma Bonza, wakati akizungumza na wananchi pamoja na wafanyabiashara hao, ambapo amewataka kila mmoja kutambua kuwa anayo nafasi ya kulinda amani na utulivu uliopo nchini kwa kushirikiana na viongozi wa serikali pamoja na Jeshi la Polisi katika kuripoti viashiria vya uvunjifu wa amani.
SSP Bonza amewataka pia wafanyabiashara wa mifugo kutokukwepa kulipa ushuru wa serikali katika biashara yao, pamoja na kuzingatia uhalali wa mifugo inayoingia na kutoka mnadani wakati wote, huku akiwataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii katika shughuli za kuwanufaisha pekee na sio katika kusambaza taarifa za uvunjifu wa amani
Naye Mkuu wa Oparesheni kutoka katika kikosi hicho Mrakibu wa Polisi (SP) Mtenga ameongeza kwa kuwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Kikosi hicho katika kuripoti viashiria uhalifu wa mifugo ikiwa ni pamoja na wizi pamoja na usafirishaji unaokiuka haki za wanyama.




Post a Comment