AFISA TARAFA KATERERO AENDELEA NA ZIARA YA KUPITA KITONGOJI KWA KITONGOJI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, KUHIMIZA ULINZI NA USALAMA N.K


 Ziara yajikita pia kueleza wananchi kuhusu shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali, miradi, sera za uwezeshaji wananchi kiuchumi n.k._


Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera ina Kata 11, Vijiji 37 na Vitongoji 159. Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku kati ya tarehe 25 hadi 28, Mei 2026 ameendelea na ziara ya kupita Vitongojini kwenye Mikutano ya Vitongoji kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kuzitatua, kuzitolea ufafanuzi na zile za kufikisha kwenye mamlaka au vitengo husika.


Ziara hii ya Afisa Tarafa Katerero imejikita pia kuhamasisha wananchi kuhusu masuala ya ulinzi na usalama kwenye maeneo yao huku Afisa Tarafa Bwanku akichangia vifaa kama tochi ili vitumike kwenye ulinzi wa usiku (sungusungu) pamoja na kuwaeleza wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo miradi, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na sera mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao. 


Tarehe 25 ziara ilifanyika Kitongoji cha Busaizi, Kijiji Kibona Kata ya Ibwera, tarehe 26 ikawa zamu ya Kitongoji cha Bituntu, Kijiji Buganguzi Kata ya Bujugo na tarehe 28 ikawa zamu ya Kitongoji cha Bwanshoni, Kijiji cha Kanazi Kata ya Kemondo. Kazi ya kuendelea kufika Vitongoji vingine inaendelea.



Post a Comment

Previous Post Next Post