🗓️ 10 MEI 2026
📍 MBEZI LUIS, UBUNGO – DAR ES SALAAM.
Mapema jana, Ndugu Masudi Mbaruku Masudi (Lopenga) ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Mshikamano, alishiriki kama Mgeni Rasmi katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Madereva Pikipiki wa Maduka Tisa, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mshikamano.
Hafla hiyo iliambatana na zoezi la ugawaji wa misaada kwa watoto wenye uhitaji maalum kutoka Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Ndugu Masudi Mbaruku Masudi alisisitiza umuhimu wa huduma bora kwa maafisa usafirishaji kwenye jamii, nidhamu, uwajibikaji na elimu kwa watoto.
JMT - KAZI IENDELEE 🇹🇿.
Wasiliana na Habarika24 kupitia WhatsApp kwa namba +255784747478


Post a Comment