MAAGIZO YA WAZIRI MKUU YAMPA TABASAMU AHMED MALUMBA

Mwananchi, Ahmedi Malumba, aliyewasilisha malalamiko yake mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Aprili 12, 2026 wilayani Chamwino (Mvumi) kuhusu kushikiliwa kwa gari lake na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma, hatimaye amepata haki yake. 

Aprili 27, 2026, gari hilo limerejeshwa rasmi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, ambapo pia amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni 4 kwa ajili ya kugharamia marekebisho ya vipuri vilivyobainika kuharibika.



Post a Comment

Previous Post Next Post