Aongozana na Mtendaji wa Kata, Mtendaji wa Kijiji, Afisa Kilimo, Baraza la Ardhi Kata._
Migogoro ya ardhi ni moja ya kero kubwa inayosumbua jamii kwenye nchi yetu. Kwasasa Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku ameweka nguvu kubwa na kutumia maarifa yake yote kusuluhisha migogoro hii ya ardhi na kuendelea kuimaliza kadri inavyowezekana kila siku ili kujenga jamii yenye amani, upendo na mshikamano.
Na leo Ijumaa Mei 29, 2026, Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku ametumia masaa 7 kusuluhisha mgogoro wa ardhi kwenye Kitongoji cha Kibirizi, Kijiji Mashule, Kata ya Kyamulaile na kufanikiwa kufanya suluhu ya mgogoro huo na kuumaliza huku pande zote mbili zikishikana mkono.
Ndugu Bwanku akiwa na Kaimu Mtendaji wa Kata ya Kyamulaile Ndugu Alex Kileo, Mtendaji wa Kijiji cha Mashule Bi. Grace Bahati, Afisa Kilimo Ndugu Joram Bombo pamoja na Uongozi wa Baraza la Ardhi Kata ukiongozwa na Mwenyekiti wake Faustine Katakweba walifanya kikao kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata Kyamulaile na baadae kufika eneo la mgogoro wa ardhi huo kisha kuusuluhisha na pande zote kushikana mikono.Ndugu Bwanku kwenye utatuzi wa migogoro amekua akisisitiza sana pande zote kuwa na utayali wa kumaliza migogoro, kutokua na misimamo mikali, kuondoa dhana ya ushindi kwa asilimia 100 na kukubali kupoteza kidogo pamoja na kutanguliza upendo ili kurahisisha usuluhishi na jamii kuendelea kuwa na amani, upendo na mshikamano.
![]() |





Post a Comment