NAIBU WAZIRI AYOUB AHIMIZA USHIRIKIANO WA WADAU NA WABUNGE KATIKA UJENZI WA VITUO VYA POLISI


 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ametoa wito kwa Wadau wa Maendeleo na Waheshimiwa Wabunge kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha miundombinu ya Usalama, ikiwemo ujenzi wa vituo vya Polisi, ili kuhakikisha huduma za Kipolisi zinawafikia wananchi kwa ukaribu zaidi


Akizungumza leo mara baada ya ukaguzi wa Mradi wa Kituo Kipya cha Polisi chenye hadhi ya daraja B, wilayani Kibiti mkoani Pwani, Mhe. Ayoub alisema kuwa pamoja na Serikali kuendelea na mpango wa ujenzi wa vituo vya Polisi kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ushiriki wa wadau na Wabunge unaweza kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo muhimu ya kiusalama.


Kadhalika, Ameeleza kuwa kila jimbo lina mahitaji ya Vituo vya Polisi, hivyo ni muhimu kwa Wabunge kutumia sehemu ya fedha za mifuko ya Majimbo kusaidia ujenzi au ukamilishaji wa vituo katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.


Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, Wabunge, Wadau wa Maendeleo na wananchi utawezesha kupunguza changamoto kwa baadhi ya Maeneo yenye umbali wa wananchi kufuata huduma za hizo


Post a Comment

Previous Post Next Post