Mwanaharakati wa utalii jumuishi, Deogratius Chami, akiwa ni mwenye ulemavu wa miguu ameanza safari ya siku sita ya kupanda Mlima Kilimanjaro akilenga kufika Uhuru Peak, katika jitihada za kuhamasisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika sekta ya utalii nchini.
Safari hiyo inalenga kuonyesha kwamba watu wenye changamoto za viungo wanaweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za utalii na kufikia malengo makubwa kama wengine.


Post a Comment