DARNES SALAAM
Na Pilly Kigome-
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amewataka wazazi kushirikiana na Serikali katika kukuza taaluma ya elimu kwa kuweka utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kutopuuza wito pindi wanapohitajika mashuleni.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es salam alipokuwa akizungumza katika kikao kilichowakutanisha madiwani na kamati ya afya ya jiji la Dar es Salaam.
Mbali na hilo amewataka maafisa afya na elimu waende wakatoe elimu ya lishe na maadili aktika ngazi ya shule za msingi na sekondari ili kukuza sekta hiyo kwa wanafunzi wake.
Amefafanua Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoafedha nyingi ili kuhakikisha kuwe na ufaulu mzuri hivyo wanawajibu kwenda kutengeneza mazingira wezeshi kufikia ufaulu huo ikiwemo na kuboresha maadili ya watoto.
“Sisi jukumu letu kama Serikali tuna wajibu wa kubadilisha tabia za wazazi na wanafunzi ili kufikia lengo la kuboresha sekta ya elimu, tunaona wanafunzi wanajiingiza kwenye mapenzi na mambo mengine ambayo hayastahili wazazi wanapoitwa hawaji kusikiliza wito na wanatuma wawakilishi wakiwemo mahousegirl na wao wanakuwa hawafikishi ujumbe vizuri kama inavyotakiwa” amesema
“Leo tumekubaliana kushuka chini twende kwenye shule za msingi na sekondari kutoa elimu ya maadili na lishe kwa watoto wetu kwani huo ndio msingi wa elimu bora”


Post a Comment