MBUNGE ONESMO MNKONDYA NA KISHINDO CHA USHINDI WA CCM, UCHAGUZI MDOGO UDIWANI KATA YA SHIWINGA, MBOZI - SONGWE


Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoa wa Songwe, Mhe. Onesmo Mnkondya ameongoza mamia ya wananchi wa Kata ya Shiwinga kuleta ushindi katika uchaguzi mdogo wa Diwani katika Kata ya Shiwinga uliofanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata ya Shiwinga, Lusekelo Mwalukomo na ambapo kwa sasa aliyeshinda nafasi hiyo ni ndugu Mzumbwe


Kampeni za Uchaguzi huo zilihitimishwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe pamoja na Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza kumuombea kura Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM ambaye baada ya Uchaguzi kufanyika Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM aliibuka na ushindi wa kishindo.


Aidha, katika kipindi chote cha kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Udiwani, Mbunge Mnkondya aliongozana na Kamati za Uchaguzi kuhakikisha Mgombea Udiwani anayetokana na CCM anashinda kwa kishindo

Post a Comment

Previous Post Next Post