Meneja wa Huduma za Utangazaji, Mhandisi Andrew Kisaka akitoa wasililisho lilohusu Matokeo na Utekelezaji wa Mapendekezo yatokayo na Utafiti wa Huduma za Utangazaji Nchini katika Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji 2026 Februari 12, 2026 Jijini Dodoma.
..................................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji 2026 umeanza rasmi kwa mawsilisho yaliyowasilishwa na wawasilishaji wabobezi katika Ukumbi wa Mikutano wa New Generation Jijini Dodoma huku ukitoa mwanga wa utatuzi wa baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Akifungua mkutano huo Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma amesema Serikali imesikia na kuzitatua changamoto za muda mrefu ikiwemo kupunguza ada za usajili ili kuwezesha vyombo vingi kuwa na usajili na kutoa Habari zenye tija kwa jamii.
Alisema usajili wa Blog ada ya kuomba ni Sh. 1O,000 na ada ya mwaka itakuwa Sh. 50,000.
Kwa upande wa Wazalisha maudhui ya online (You Tuber) ada ni Sh. 100,000 huku ada ya maombi ikiwa ni Sh.20,000.
Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo ni vyombo vya utangazaji ambavyo ni televisheni, redio na mitandao ya kijamii.
Mawasilisho yaliyowasilishwa yalikuwa matatu la kwanza likiwa ni Matokeo na Utekelezaji wa Mapendekezo yatokayo na utafiti wa Huduma za Utangazaji Nchini iliyotolewa na Mhandisi Andrew Kisaka kutoka TCRA.
Wasilisho la pili lilikuwa ni Fursa na Faida za Uwekezaji wa Teknolojia katika Utangazaji Vijijini, lililotolewa na Zuhura Selemani ambaye ni Mhadhiri Msaidizi.
Wasilisho la tatu lilihusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Huduma za Utangazaji wa Redio Vijijini (Uzoefu wa UNESCO), lililowasilishwa na Mhadhiri Dkt. Egbert Mkoko kwa niaba ya Nancy Mwaisaka kutoka UNESCO.
Mkutano huo wa siku mbili ambao umeanza leo Februari 12, 2026 Jijini Dodoma utafikia tamati kesho Februari 13, 2026 na umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa habari nchini.
Mhadhiri Msaidizi Zuhura Selemani akitoa Wasilisho Kuhusu Fursa na Faida za Uwekezaji wa Teknolojia katika Utangazaji Vijijini.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.Mkutano ukiendelea.Wadau wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huoMkurugenzi wa Taasisi ya Wanahabari Kusini Mwa Africa (MISA-TAN), Elizabeth Riziki akichangia jambo kwenye mkutano huo.Mkutano ukuiendelea.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, William Shao wakiwa kwenye mkutano huo.Waandishi wa Mitandao ya Kijamii (Blogers) wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Programu Manager Kisaco Media, Emele Mwaipopo, Mkurugenzi wa Madelemo Nes, Lilian Madelemo na Miga picha wa Kujitegemea, Swaum Said.Wamiliki wa Blogs wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Othman Maudi Mwendeshaji wa Blog ya Zanzibar News, Mr. Verbs Mkurugenzi Mtendaji wa Habarika24 Blog, na Cathebat Kajuna Mwendeshaji wa Blog ya Kajunason..Mtaangazaji Nguli, Abdalla Kajura akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Post a Comment