
Kutana na Kisali Simba, Mshiriki wa Programu ya YALI Mandela Washington Fellowship 2025 kutokaTanzania na mwandishi wa habari aliyeshinda tuzo mbalimbali, pia mtetezi wa usawa wa kijinsia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 11 katika tasnia ya habari.
Kwa sasa ni Mhariri wa Vipindi na Makala wa Star TV Tanzania, ambapo anatumia jukwaa lake kuinua sauti za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu. Kisali pia ni mwanzilishi mwenza wa Mwanamke Imara, asasi isiyo ya kiserikali inayojikita katika kuelimisha jamii na kupambana na ukatili wa kijinsia kote Tanzania.
Uandishi wake wenye ushawishi mkubwa umemletea tuzo za kitaifa na kimataifa katika maeneo ya haki za wanawake, kilimo, na mazingira. Kisali anashiriki fellowship yake ya Uongozi katika Ushiriki wa Kiraia katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan (Michigan State University).
🧠Anatumia nguvu ya vyombo vya habari kuleta mabadiliko ya kijamii na kutetea haki.
……………………………..............
Kisali Simba.
Meet Kisali Simba, a 2025 🇹🇿 YALI Mandela Washington Fellow and award-winning journalist and gender advocate with over 11 years of experience in the media industry.
She currently serves as Features and Program Editor at Star TV Tanzania, where she uses her platform to amplify the voices of women, children, and people with disabilities. Kisali is also the co-founder of Mwanamke Imara, an NGO working to raise awareness and fight Gender-Based Violence across Tanzania.
Her powerful storytelling has earned her national and international awards in women’s rights, agriculture, and the environment. Kisali is hosted by Michigan State University for her fellowship in Leadership in Civic Engagement.
🧠She’s using the power of media to drive social change and advocate for justice.
#YALI2025
@_beingkisali_
Post a Comment