Huku wawakilishi wa michuano hiyo kutoka Tanzania ikiwa ni klanu ya Simba kwa michuano ya kombe la Shirikisho na Yanga kwa klabu bingwa Afrika.
Kombe la shirikisho Afrika 2024/2025
Jana jumapili ya tarehe 08 Disemba 2024 michuano ya mzunguko wa pili iliendelea huku wekundu wa msimbazi Simba SC wakiwa ugenini Algeria wakiwakabili CS Constantine na matokeo yaliisha kwa Simba kupoteza mchezo huo kwa kufungwa Goli 2 kwa 1.
- Mchezo wa kwanza wa Simba uliofanyika jijini Dar es Salaam dhidi ya F.C. Bravos do Maquis Simba aliibuka na Ushindi wa goli moja kwa 0.
- Kwa matokeo hayo Simba SC amejikusanyia pointi 3 na kumfanya kua katika nafasi ya 3, huku kundi likiongozwa na CS Constantine kwa pointi 6.
Msimamo wa Kundi A la Simba SC Kombe la Shirikisho Afrika
Klabu Bingwa Afrika 2024
Upande mwingine klabu ya Yanga inayoshiriki michuano ya klabu bingwa Afrika kwa msimu huu wa 2024/2025 ilikua ugenini Algeria ikivaana na MC Alger na kujiukuta ikipoteza mchezo huo kwa kupokea kichapo cha goli 2 kwa 0
- Yanga hadi sasa imecheza michezo 2 na kupoteza michezo yote, kuifanya iwe katika nafasi ya 4 ikiwa na jumla ya point 0 kwenye kundi A ambalo linaongozwa na AL Hilal mwenye jumla ya point 6.
Post a Comment