ISOC-Tz Yaibuka Namba Moja Tuzo Za WSIS 2024 PRIZES, Matumizi Ya Interneti Isiyo Na Mipaka


                                                                                     Rais wa ISOC Tanzania, Nazar Kirama

TAASISI ya internet Society Tanzania Chapter (ISOC-TZ) imeibuka kidedea namba moja baada ya usaili wa project 1049 toka pande za dunia baada ya usaili wa project 369 zilizoingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya matumizi ya internet usio na mipaka.

ISOC-Tz imeibuka namba moja kwa kuwakilisha project yao ijulikanayo kama TANZANIA DIGITAL INCLUSION PROJECT inayotekelezwa katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar Es Salaam.

Rais wa ISOC Tanzania Nazar Kirama (katikati) akipokea tuzo hiyo, kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Tuzo hizo zilizofanyika Geneva nchini Uswiss zinazojulikana kama World Summit on Information Society (WSIS 2024 PRIZES) ISOC -TZ ilifanikiwa kupitia katika ‘kategori’ tatu.

Hayo ameyasema Rais wa ISOC Tanzania, Nazar Kirama baada ya usaili wa mradi wa matumizi ya Internet usio na mipaka ‘Tanzania DIgital Inculusion’ nchini Uswis Geneva. Amesema jumla ya projects zilizosailiwa zilikuwa 1049 toka pande zote za Dunia.

Aidha amesema Baada ya usaili project 360 tu ndio ambazo zimeingia kwenye kinyang’anyiro. Project yetu ni kati ya hizo project 360 ambazo ndizo wagombea wa TUZO ZA WSIS 2024.

Tuzo hiyo imepokelewa na Rais Wa ISOC -Tanzania aliyeongozana na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ambapo kwa pamoja walishukuru Watanzania wote kwa ushirikiano waliouonyesha wakati wa mchakato wa upigaji kura uliokuwa unafanyika kwa njia ya kimtandao (online) kwani hakuna mtu atayeachwa nyuma.

“Naamini tuzo hii siyo ya Isoc Tanzania ni ya Watanzania wote walioweza kuonyesha mwanzo mzuri kwani hakuna mtu atayeachwa nyuma, tutaendeleo na ushirikiano tulioweza kuuonyesha,” alisema Kirama na kuongeza nashukuru kwa kuwa nimeweza kupokea tuzo hii pamoja na Waziri wa wizara husika ni imani kubwa sana kwamba Tanzania tutaendelea kufanya vizuri zaidi.


Post a Comment

Previous Post Next Post