ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WAH. WABUNGE LAFANYIKA DODOMA

Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akiwa na Afisa Usajili Bw. Surera wakati akipata huduma ya usajili kwenye ukumbi wa Bunge. Katika zoezi hilo mbali na kujaza fomu za maombi ya Utambulisho, pia walichukuliwa alama za kibaiolojia picha na saini ya kielektroniki.
…………………………………………………………………………………………..
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), imeanza kusajili Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; wakati wakiendelea na kikao cha Bajeti
Katika Usajili huo NIDA inategemea kusajili wabunge wote ambao hawakuwahi kusajiliwa awali na kupata vitambulisho vya Taifa, pamoja na kugawa vitambulisho
Wabunge wameonyesha mwamko mkubwa katika kutumia fursa hii adhimu, kwa kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele kutimiza haki yao ya kikatiba ya kusajiliwa na kupata kitambulisho cha Taifa; ambacho kimekuwa na faida nyingi kiuchumi, kijamii na kisiasa

Mpaka sasa NIDA imeshatoa zaidi ya  vitambulisho zaidi ya milioni 2.5 na kwa sasa NIDA iko mbioni kuanza usajili kwa kutumia mtaji wa taarifa toka NEC ambapo zaidi ya wananchi milioni 22 watasajiliwa na kupewa namba ya utambulisho ili kuanza matumizi mbalimbali
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. Saed Kubenea akisaidiwa kujaza fomu za maombi za Vitambulisho vya taifa na Afisa Usajili Bi. Hadija Bauji.
Mh. Saed Kubenea akisaidiwa na Afisa Usajili Bw. Surera kuchukua alama za vidole wakati wa hatua ya uchukuaji alama za kibaiolojia.
Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akisaidiwa kujaza fomu na Meneja Usajili Vitambulisho vya Taifa, Bi. Julian Mafuru


Post a Comment

Previous Post Next Post