KASHFA YA RUSHWA YA SABABISHA ZITTO AJIUZULU UJUMBE WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII.

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe.

Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameishtumu Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe hupokea rushwa.

Kutokana na shtuma hizo ameamua kumuandikia spika kumtaka achunguze na kuchukua hatua.

Kauli yake ianapatikana hapa chini;
"Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika." Zitto Kabwe


Zitto Kabwe amechukua uamuzi huu baada ya leo Gazeti la Mtanzania kuandika tuhuma zenye ushahidi juu ya rushwa kwa kamati mbalimbali za Bunge ikiwepo Kamati ya Zitto Kabwe.Uamuzi huu umekuja ili kuenzi falsafa ya chama cha ACT ambayo ni UTU,UZALENDO NA UADILIFU.

Post a Comment

Previous Post Next Post