SERIKALI: MADUKA YOTE YA DAWA YALIYO NJE YA HOSPITAL ZA SERIKALI MARUFUKU

Maduka yote ya dawa nje ya hospitali za Serikali kuondolewa.

Ni mkakati wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa kukomesha wizi wa dawa unaofanywa na watumishi wasio waaminifu.

Katibu mkuu Dk. Donald Mmbando amesema tayari wameandaa rasmi rasimu ambayo imeshakamilika wanasubiri Waziri wa Afya atakayeteuliwa aweze kuipitisha.

Adai Serikali pia inatarajia kutoa bei elekezi ya matibabu katika hospitali zote za binafasi ili mwananchi aweze kumudu gharama za matibabu.

Aiagiza MSD kuhakikisha inaweka dawa za kutosha kwenye hospitali wakati wote "naomba iwe mwisho kusikia mgonjwa anaenda kununua dawa nje, eti kisa hospital haina dawa, natamka sitaki kusikia tena'.

Chanzo: Magic Fm NA JAMIIFORUMS

Post a Comment

Previous Post Next Post