ZIARA YA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP ERNEST MANGU -MKOANI PWANI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ,IGP Ernest Mangu akikagua gwaride lililo andaliwa kwa ajili yake  wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Pwani .IGP alikuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo alizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari  wa mkoa huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGPErnest Mangu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Evarest Ndikilo wakati alipomtembelea ofisini kwake wakati alipokuwa katika  ziara yake ya kikazi mkoani Pwani .IGP alikuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo alizungumza pia na na Maofisa, Wakaguzi na Askari  wa mkoa huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Bw.Bravo Ryapambile (katikati) wakati alipokuwa katika  ziara yake ya kikazi katika wilaya hiyo ambapo alikagua baadhi ya vituo vya polisi vilivyopo katika wilaya hiyo.Kushoto ni Mkuu wa Polisi Wilayani Mkalama, Mrakibu wa Polisi  Michael Marwa.
                                           Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi

Post a Comment

Previous Post Next Post