KAMPUNI
ya ACACIA inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, imezindua
kampeni ya kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, leo Jumatatu Juni
22, 2015, ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia sekta ya elimu kwenye maeneo
yanayozunguka migodi mitatu inayomilikiwa na kampouni hiyo ya North Mara,
Bulyanhulu na Buzwagi.
Kundi la watu 21, wakiwemo, wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro Juni 22, 2015
Akizungumza
muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwenye lango
la Machame,iliyo shirikisha watu 21, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Brad
Gordon, alisema, kampuni yake ilianzisha mpango ujulkikanao kama “CAN EDUCATE”,
ikimaanisha tunaweza kujieleimisha, imeamua kukusanya fedha kupitia kupanda
mlima Kilimanjaro, ili kusaidia elimu na kampuni inimekuwa ikifanya hivyo kila
mwaka.
“Lengo
ni kukusanya dola za Kimarekani 200,000, zitakazosaidia jamii inayokaa
kuzunguka maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo” alisema Meneja Mkuu
wa Uendelezaji wa Kmapuni, Asa Mwaipopo.
Na
kuongeza kuwa kuna watoto wengi wanashindwa kendelea na elimu ya sekondari na
ile ya chuo kikuu, sio kwa sababu za uwezo mdogo wa kimasomo, bali ni ukosefu
wa fedha za kuendelea na elimu.
Acacia imeamua kushiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili watimize ndoto zao. Alimaliza Mwaipopo. Pichani,
Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya ACACIA, Brad Gordon, (Wapili kushoto),
akiongoza timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi, marafiki na familia za
wafanyakazi wa kampuni hiyo ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame
mkoani Kilimajaro Jumatatu Juni 22, 2015, kwa lengo la kuchangisha fedha kwa
ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini.
Acacia imeamua kushiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili watimize ndoto zao. Alimaliza Mwaipopo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (katikati), akiwa na Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuongoza timu ya wapanda mlima Kilimanjaro kwa nia ya kukjsuanya fedha hizo
Brad, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Necta Pendaeli Foya (katikati)
(Habari na K-VIS MEDIA, picha na Dixon Busagaga).
(Habari na K-VIS MEDIA, picha na Dixon Busagaga).
Post a Comment