Mkurugenzi wa Mipango na Tehama wa Ofisi ya Bunge Sigfred Kuwite akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akieleza vifaa vilivyotolewa na
Serikali ya China kupitia Ubalozi wake hapa nchini kwa ajili ya kusaidia
Bunge kutekeleza majukumu yake.
Balozi
wa China hapa Nchini Mhe. Dkt. LU Youquing akizungumza wakati wa hafla
ya kukabidhi vifaa hivyo vya TEHAMA kwa Ofisi ya Bunge.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea kutoka kwa Balozi wa China hapa
Nchini Mhe. Dkt. LU Youquing baadhi ya Vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa
serikali ya China kwa ajili ya kusaidia shughuli za Bunge.
Vifaa hivyo
vyenye thamani ya Dola za Kimarekani laki moja vimekabidhiwia leo katika
hafla iliyofanyika Ofisi ya Spika jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akizungumza kutoa neno la shukrani mara baara ya kupokea vifaa hivyo.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea zawadi ya kitabu kilichoandikwa na
Rais wa China kutoka kwa Balozi wa China hapa Tanzania Mhe. Dkt. LU
Youquing mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Dkt. LU
Youquing na viongozi wengine wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA
Picha na Owen Mwandumbya .
Post a Comment